Jumatatu , 22nd Nov , 2021

Mchezaji wa Olympique Marseille, Dimitri Payet amekuwa muhanga kwa mara nyingine baada ya kurushiwa chupa na mashabiki wa Olympique Lyon katika dabi iliyohailishwa baada ya dakika tano tu mchezo kuanza usiku wa jana.

(Watu wa Usalama wakiruliza ghasia)

Mwamuzi wa mechi huo Ruddy Baquet aliwaamuru wachezaji kurudi ndani ya vyumba vya kubalisha nguo na baada ya kungoja kwa muda mrefu wachezaji wa Marseille hakurdi tena kiwanjani, hali iliyopelekea kuhairishwa kwa mchezo huo.

Hii ni mara ya pili msimu huu Payet kupigwa na chupa huku kukiwa na mfululizo wa matukio katika soka la Ufaransa.

Mechi ya Marseille dhidi Nice mnamo Agosti mwaka huu ilifutwa wakati kiungo huyo wa zamani wa West Ham aliporusha chupa kwenye umati, na kusababisha mashabiki kuvamia uwanja

Nice walikatwa pointi mbili, na mashabiki wakifungiwa mechi moja kuingia uwanjani huku Payet akifungiwa mchezo mmoja.Kiungo wa kati wa Marseille Valentin Roniger aliimia mdomo alipopigwa na chupa kwenye mechi ya ufunguzi wa msimu walipocheza na Montpellier.

Na nusu ya pili ya derby ya kaskazini kati ya RC Lens na Lille mnamo Septemba ilichelewa kwa karibu nusu saa baada ya mashabiki wa wapinzani kurushiana vitu.

Kisha watu walikimbilia uwanjani, na kusababisha polisi wa kutuliza ghasia na wasimamizi kuingilia kati.