Jumanne , 29th Dec , 2015

Shirikisho la Riadha Tanzania RT limesema, viongozi wa mikoa wanachangia kushusha mchezo huo hapa nchini kutokana na udanganyifu katika mashindano mbalimbali hapa nchini.

Kaimu katibu mkuu wa RT Ombeni Zavara amesema, viongozi wa mikoa huchangia kushusha kwa mchezo huo hapa nchini kwa wengi wao kuchagua wachezaji wachache kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mikoa na wengine kununua wanariadha kutoka mikoa mingine kwa ajili ya kushiriki mashindano nje ya mkoa wake.

Zavara amesema, pamoja na viongozi kushusha nchezo huo lakini pia udhamini umechangia suala linalochangia chama kushindwa kuwa na mashindano mbalimbali ambayop yangechangia kuweza kupata vijana ambaon wangeweza kuunda timu ya Taifa ya vijana ambao hapo baadaye wangeweza kufanya vizuri pia kama ilivyo kwa wanariadha wengine wa nchi mbalimbali.