
Akizungumza na East Africa Radio, Katibu wa Klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya, Daudi Kilo amesema, wakiwa wanahitaji mchezaji wasimuangalie katika mashindano ya muda mnfupi na kuona anafaa bila kujua uwezo wake ambapo hapo baadae wanaachana nae na kulalamika kuwa kiwango chake sio kizuri.
Kilo amesema, mashindano ya muda mfupi sio kipimo kizuri kwani wioki moja au mbiuli haifanyi mchezaji kuwa mzuri anapokuwa Uwanjani9.
Kilo amesema, Tanzania itakapohitaji mchezaji hawawezi kuwazuia lakini wanatakiwa kuangalia uwezo wake kutokana na nafasi aliyonayo katika klabu yake.
Kilo amesema, kwa kipindi hiki hawawezi kumuuza mchezaji kwani dirisha la usajili limeshafungwa na watakapomuuza mchezaji mmoja itawapa shida katika kikosi hicho kwani itawalazimu wasubiri hadi kumalizika kwa msimu ndipo wasajili.