Ijumaa , 2nd Jul , 2021

Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique amesema anatagemea kupata ushindani mkubwa dhidi ya timu ya Uswisi kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya Euro 2020, mchezo utakao chezwa leo Saa 1:00 Usiku katika dimba la Krestovsky St Petersburg,Urusi.

Luis Enrique

"Jambo zuri kwetu ni kwamba timu zote zinajuana vizuri sana, Tulishindana hivi karibuni kwenye michuano ya UEFA Nation league. Ni timu ngumu kukutana nayo, ngumu sana kukabiliana nao nadhani kwa watazamaji sio mchezo mkubwa lakini ni timu yenye wachezaji wazuri. Wanafanana na sisi namna wanavyokaba, wanavyoshambulia itakuwa ngumu sana kwetu”. Amesema Luis Enrique

Uswisi wametinga hatua ya robo fainali ya michuano hii baada ya kuwatoa mabingwa wa Dunia timu ya taifa ya Ufaransa kwa michwaju ya penati 5- 4 kwenye mchezo wa 16 bora baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 ndani ya dakika 120.

Hispania walikata tiketi kwa kuifunga timu ya taifa ya Croatia kwa ushindi wa mabao 5-3 kwenye mchezo ambao uliochzwa dakika 120 baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 3-3 ndani ya dakika 90 na baadae Hispania ikafunga mabao 2 kwenye dakika 30 za ziada.

Huu utakuwa ni mchezo wa kwanza timu hizi zinakutana katika michuano ya mataifa barani ulaya Euro, na kwenye mashindano makubwa wamekutana mara tatu mwaka 1966, 1994 na 2010 kwenye fainali za kombe la Dunia. Uswiss wameshinda mara moja na Hispania wameshinda michezo miwili.

Mshindi wa mchezo huu atafuzu hatua ya nusu fainali na atacheza na mshindi wa mchezo mwingine wa robo fainali kati ya timu ya taifa ya Italia na Ubeligiji.