Jumatano , 18th Jun , 2014

Wazazi nchini Tanzania wameashauriwa kutowazuia watoto wao kushiriki katika michezo mbal mbali ikiwemo ile ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi UMITASHUMTA kwa lengo la kuinua vipaji vya michezo kwa watoto hao.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi DSM wakiwa katika mashindano viwanja vya Chuo Kikuu

Wito huo umetolewa na Mratibu wa michezo ya UMITASHUMTA Kanda maalum ya Dar es salaam Isac Richard wakati alipokuwa akizungumza na Muhtasari wa michezo, huku timu mbali mbali ikiwemo ya Netbal itakayoshiriki mashindano hayo ikiwa imepiga kambi na kuendelea na mazoezi.

Amesema baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kuwazuia watoto wao kushiriki katika michezo hiyo kwa madai kwamba watakosa masomo jambo ambalo amesema si sahihi kwa kuwa michezo hiyo ipo kwa kipindi maalum.