Jumatano , 29th Jun , 2016

Mshambuliaji wa klabu ya TP Mazembe ya DR Congo amesema wapinzani wao wa jana klabu ya Yanga bado ina nafasi ya kuingia nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika kwa kuwa kuna mechi ambazo endapo watashinda watatimiza lengo lao.

Thomas Ulimwengu(kushoto)akipokea maelekezo kutoka kwa kocha wake.

Ulimwengu raia wa Tanzania amesema kwa namna Yanga wanavyocheza wanaonekana wamejiandaa kikamilifu japo kuwa kukosekana kwa uzoefu wa mashindano wa kimataifa kwa wachezaji wake ndiko kunakopelekea kushindwa kupata matokeo.

Nyota huyo amekiri kukutana na wakati mgumu sana katika mchezo wa jana lakini wakaonesha nini thamani ya wachezaji wa kulipwa jambo lililowapa ushindi wa bao moja kwa sifuri wakiwa ugenini.

Mazembe imekamata usukani wa kundi A ikiwa imejikusanyia alama sita kwenye michezo miwili ya awali huku Yanga ikiendelea kushikilia nafasi ya mwisho katika kundi lake.