Jumatano , 1st Jul , 2015

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba Sc Shaban Kisiga amesema, ukorofi alionao ndio umemsababisha kusajiliwa na Ruvu Shooting na akaachana na timu zanye mashabiki wengi.

Katika taarifa yake, Kisiga amesema, ameamua kujiunga na maafande hao na kuepusha vurugu kwa timu zinazoshiriki Ligi kuu ambapo kwa sasa anaamini yupo sehemu tulivu na yenye usalama zaidi.

Kisiga amesaini mkataba wa mwaka mmoja juzi katika klabu hiyo ya Ruvu Shooting ambayon ilishuka Daraja na sasa ipo daraja la kwanza.