Taarifa ya chama cha soka nchini Italia FIGC imesema wachezaji hao hawana hali nzuri ya kushiriki kwenye michezo miwili dhidi ya Malta na England kwa ajili ya kufuzu michuano ya Ulaya 2024 nchini Ujerumani na hivyo wameruhusiwa kurejea kwenye klabu zao.
Mapema Alhamisi Oktoba 12-2023 Waendesha mashtaka wa FIGC walitangaza uchunguzi dhidi ya kiungo wa Juventus Nicolo Fagioli kuhusu na ushiriki wake usivyo halali wa kubashiri mitandaoni huku Italia ambao ni bingwa mtetezi wa michuano ya Ulaya inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi C wakiwa na alama 7 mpaka sasa.