Jumatano , 4th Nov , 2015

Shirikisho la ngumi za kulipwa nchini TPBC limesema linatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa chama hicho mwakani.

Rais wa TPBC Parasa Chaurembo amesema, walitarajia kufanya uchaguzi mkuu ndani ya mwaka huu lakini kutokana na muingiliano wa ratiba hususani uchaguzi mkuu wa nchi wameamua kuuanza mwaka kwa kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi katika chama hicho.

Chaurembo amesema, viongozi waliopo sasa ni wa muda hivyo uchaguzi wa mwakani utahusisha viongozi wa ngazi mbalimbali katika chama hicho ambao wanaamini wataendeleza maendeleo yaliyopo ndani ya chama hicho.