Ijumaa , 19th Jun , 2026

Kiungo wa Canada, Ismaël Koné, amepata jeraha kubwa la kuvunjika mguu kufuatia rafu mbaya aliyofanyiwa na mchezaji wa Qatar, Assim Madibo.

Baada ya tukio hilo, Madibo alionyeshwa kadi nyekundu huku Koné akitolewa uwanjani kwa machela, katika mchezo huo ambao Canada iliibuka na ushindi mabao 6-0 dhidi ya Qatar kwenye michuano ya Kombe la Dunia.