Baadhi ya wachezaji wa tenisi kwa walemavu wakiwa katika mafunzo.
Kwa upande wao chama cha mchezo wa tenisi Tanzania TTA hali imekuwa tofauti mara baada ya vifaa vya mchezo huo kukwama bandarini kwa muda mrefu sasa kutokana na chama hicho kukabiliwa na ukata na kukosa fedha za kukombolea vifaa hivyo walivyotumwa kwa msaada wa chama cha mchezo huo duniani FINA hivyo kupelekea vijana wengi hasa chipukizi kukosa fursa ya kupata mafunzo kwa vitendo msimu huu.
Kocha wa tenisi ambaye ni mratibu wa mchezo huo nchini kupitia chama cha tenisi Tanzania TTA Salum Mvita amesema kukosekana fedha za kuvitoa vifaa hivyo kwa kiasi kikubwa kumeleta changamoto kwa wakufunzi na wachezaji kwa ujumla kufanyia mazoezi kwa vitendo.
Mvita amesema mwaka huu pia umekuwa si wamafanikio sana kwa mchezo huo hapa nchini hasa kutokana na mambo mengi kugubika mchezo huo kuanzia ndani ya chama, wanachama shiriki vilabu na mikoa hadi nje kubwa ni kukosa fedha za kukamilisha mambo mbalimbali ya kimchezo ikiwemo kukomboa vifaa hivyo lakini pia kuendesha mafunzo na mashindano mengi.
Akimalizia Mvita ambaye aliwahi kuwa mchezaji bora wa tenisi nchini miaka ya nyuma amesema ana matumaini makubwa kwa uongozi mpya wa Rais Magufuli na mawaziri wake kuwa michezo itafanikiwa ikiwemo suala la kufutiwa kodi ama kupewa misamaha ya kodi kwa vifaa vyote vya michezo hali itakayosaidia kuinua michezo hapa nchini kwakuwa hata wafadhili toka nje ya nchi watakuwa na moyo wa kutoa misaada ya vifaa mbalimbali kwa michezo mbalimbali.