Jumanne , 11th Jun , 2024

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salim Abdallah 'Try Again' amejiuzulu nafasi hiyo na kumuomba mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji 'Mo' kurudi kuiongoza.

Try Again amefikia uamuzi huo baada ya kuhudumu kwenye uongozi ndani ya Simba kwa takribani miaka saba ambapo minne alikuwa Mwenyekiti wa muda wa Klabu na mitatuMwenyekiti wa kuteuliwa na Bodi ya Simba.

Akizungumza jijini Dares Salaam, Try Again amesema amekaa na Mwekezaji wa Simba, MO na kumpa ripoti ya klabu hiyo wapi wamefeli msimu uliomalizika na nini wanatamani kukifanya ili timu hiyo iweze kusonga mbele.

"Kuiokoa Simba na kuitoa katika nafasi ilivopo sasa ni Mo pekee ambaye anaweza kufanya hivyo kwa kuitoa ilipo sasa na kuipeleka mbele, nimekuwa nikizungumza naye mara kwa mara hadi mara kumi lengo ni kuna anarudi kuijenga Simba imara na bora,"amesema  na kuongeza;

"Nimefanya mazungumzpo naye na kumuomba arudi kuwaMwenyekiti wa Bodi ya Simba kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, mimi nitabaki kuwa mwanachama na nitakuwa kiongozi ambaye nitakuwa tayari kuitumikia Simba wakati wowote."

Try Again alisema yeye ni mwanachama na kiongozi wa timu hiyo, ni mdogo kuliko klabu, hivyo ameamua kuachia nafasi hiyo ili kumuachia kiongozi ambaye anamuamini na anaamini ataipeleka Simba kwenye mafanikio.

"Mashabiki, wanachama wa Simba wanataka mafanikio na hata sisi viongozi tunatamani hayo mafanikio na tunaumia mara mia ya mashabiki kwa sababu sisi tunafanya uwekezaji na tunataka matokeo mazuri ili tupate sifa kutoka kwa mashabiki na wanachama, hakuna kongozi ambaye anafurahia timu kushuka kimafanikio," alisema na kuongeza;