Jumatano , 26th Nov , 2014

Timu ya Taifa ya mchezo wa kuruka kamba inatarajia kuelekea Nairobi nchini Kenya Desemba 11 kwa ajili ya michuano ya Afrika Mashariki,kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia litakalofanyika mwakani Paris,Nchini Ufaransa.

Akizungumza na East Africa Radio,Mratibu wa mashindano hayo kutoka hapa nchini,Denis Makio amesema timu hiyo inatarajiwa kuondoka nchini ikiwa na jumla ya watu 40 ambao ni wachezaji pamoja na viongozi.

Makoi amesema katikia kuhakikisha wanakuza mchezo huo hapa nchini,wameanzisha programu ya mchezo huu kwa shule takribani 20 za jijini Dar es salaam ambapo wanafunzi wengi wamejitoikeza kwa ajili ya kujifunza mchezo huu.