Coastal Union imeshinda mabao 2-0 na kufikisha alama 26 katika nafasi ya pili pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu zingine katika kundi hilo. Timu hiyo ilishuka msimu wa 2015/16.
Wakati huo timu ya KMC ya jijini Dar es salaam imefanikiwa kupanda ligi kuu baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya JKT Mlale kwenye mchezo uliomalizika jioni hii. Timu hiyo imefikisha alama 28 kileleni mwa kundi B ambalo mechi zake zimemalizika leo.
Naye kocha wa KMC Fred Felix Minziro ameweka rekodi ya kupandisha timu mbili tofauti kwa misimu miwili mfululizo baada ya kuipandisha timu ya Singida United msimu uliopita.

