
Afisa habari wa timu hiyo Wille Kulwa amesema, wametafuta wachezaji wazuri walio ndani ya Jeshi ambao wameajiriwa kwa ajili ya michezo na wanaamini watawasaidia kwa ajili ya kuiweka timu katika nafasi nzuri.
Kulwa amesema, wamecheza mechi za majaribio kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya ligi daraja la pili na kombe la shirikisho linaloanza Jumapili ya wiki hii ambapo wanaamini zitawasaidia pia kuwaweka katika nafasi nzuri na kuweza kuweka ushindani kwa timu nyingine shiriki.
Kulwa amesema, wanataka kuhakikisha malengo yao yanatimia kwani hawajajipanga kwaajili ya kuishia ligi daraja la kwanza bali wanahitaji mpaka ikifika miezi miwili ijayo waweze kucheza ligi kuu ya Soka Tanzania Bara na kuweza kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali makubwa.