
Ronaldo ametimiza miaka 33 leo hivyo ametumia siku yake ya kuzaliwa kuungana na familia yake hadi kesho jumanne ambapo Madrid wanatarajia kuendelea na mazoezi.
Uwanja wa klabu hiyo Santiago Bernabeu leo umeonekana ukiwa umejaa theluji ikiwa ni mwendelezo wa majira ya baridi na mvua katika baadhi ya nchi barani Ulaya.
Real Madrid ilitoka sare ya mabao 2-2 na Levante, kwenye mchezo wa La Liga jumamosi iliyopita ambapo mabingwa hao watatezi wamefikisha alama 39 katika nafasi ya nne.
Kwa upande mwingine mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa akifanya mazoezi kwenye mitaa ya jiji la Madrid akiwa ameongozana na mbwa wake.