![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2018/08/28/WAAMUZI 1.jpg?itok=mBRBlnO-×tamp=1535474328)
Waamuzi wa mchezo kati ya Simba na Mbeya City jana. Picha haihusiani na waamuzi waliofungiwa.
Waamuzi waliosimamishwa kupisha uchunguzi ni pamoja na mwamuzi msaidizi namba 2 (Line 2) Godfrey Msakila kutoka Geita mchezo kati ya Yanga SC dhidi Mtibwa Sugar, Msakila ambaye anadaiwa kukataa goli la Makambo kwa kudai mfungaji alikuwa kwenye eneo la kuotea.
Mwamuzi mwingine ni Sylvester Mwanga kutoka Kilimanjaro (Line 2) mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa naye amesimamishwa kwa kulalamikiwa kuzuia shambulizi la Mtibwa akidai Ismail Aidan alikuwa ameotea huku picha za video za marudio ya tukio hilo zikionyesha hakuotea.
Wengine ni Nassoro Mwinchui na msaidizi wake Abdallah Rashid wa Pwani wamesimamishwa kwa kosa la kukataa goli la Biashara United katika mechi ya Coastal Union dhidi ya Biashara wakidai mfungaji alikuwa ameotea.
Pia, Mwamuzi msaidizi Nicholas Makaranga wa Morogoro amesimamishwa kwa kukataa goli la Ruvu Shooting dhidi ya KMC akidai mfungaji Fully Zullu Maganga alikuwa kwenye nafasi ya kuotea.
Adhabu hiyo pia haijamuacha mwamuzi msaidizi Ahmada Jamada kutoka Kagera ambaye alikataa goli la kusawazisha la Mwadui FC dhidi ya Singida United juzi Jumapili kwa madai ya kuwa mfungaji alikuwa ameotea.
Aidha, Mwenyekiti wa hiyo amesema kuwa waamuzi hao walichezesha chini ya kiwango na kupata alama chache zilizopelekea kusimamishwa kwao ili kupisha uchunguzi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.