Ijumaa , 3rd Feb , 2017

Mlinzi wa Chelsea John Terry amemuelezea kiungo wa zamani wa timu hiyo, Frank Lampard, kama mchezaji gwiji ambaye hajapata kutokea ndani ya klabu hiyo.

Lampard, mwenye umri wa miaka 38, alitangaza kustaafu soka siku ya jana, baada ya kucheza kwa miaka 21, soka la ushindani.

"Ni mchezaji mkubwa katika historia ya klabu yetu kubwa ya soka" Terry aliandika kwenye Instagram.

"Kumbukumbu kubwa ni taji baada ya taji, mwaka baada ya mwaka, siwezi kusahau. Umeshinda kila kitu na unapaswa kujisifu. Aliandika Terry.

Lampard, aliyemalizia soka lake kwenye klabu ya New York City ya ligi kuu ya soka nchini Marekani, ameshinda mataji 11 na Chelsea miongoni mwa mataji hayo ni, mataji matatu ya ligi kuu ya EPL, mataji manne ya FA, mataji mawili ya kombe la ligi, taji moja la  ligi ya mabingwa 2012, na taji moja la Europa League.