Jumatatu , 20th Apr , 2015

Semina ya Makocha wakufunzi inatarajiwa kufanyika Aprili 27 mpaka Mei mbili mwaka huu jijini Dar es salaam huku ikiwajumuisha jumla ya makocha wakufunzi 21.

Katika taarifa yake, Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, watakaohudhuria semina hiyo na leseni zao ni; Michael Bundala (A) Ilala, Leodgar Tenga (A) Kinondoni, George Komba (A) Dodoma, Don Korosso (A) Kyela-Mbeya, Wilfred Kidao (B) Ilala, Rogasian Kaijage (A) Mwanza, Mkisi Samson (B) Mbeya, Dr. Mshindo Msolla (A) Kinondoni, Ally Mtumwa (A) Arusha, Madaraka Bendera (A) Arusha.

Wengine ni Juma Nsanya (A) Tabora,  Hamim Mawazo (A) Mtwara, Wanne Mkisi (B) Kinondoni, Major Abdul Mingange (A) Kinondoni, Dr. Jonas Tiboroha (C) Ilala, Nasra Mohamed (A) Zanzibar, John Simkoko (B) Morogoro, Juma Mgunda (B) Tanga, Triphonia Temba (B) Manyara, Ambonisye  Florence (C) Pwani, na Eugen Mwasamaki (B) Dar es salaam.