Jumanne , 13th Oct , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania ya tenis ya walemavu inakabiliwa na uhaba wa vifaa kwa ajili ya maandalizi yao kuelekea michuano mbalimbali ya Kimataifa.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya tenis ya walemavu inakabiliwa na uhaba wa vifaa kwa ajili ya maandalizi yao kuelekea michuano mbalimbali ya Kimataifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kocha mkuu wa timu hiyo Riziki Salum amesema kukosekana kwa baadhi ya vifaa kama viti vya kukaa (Wheel Chair) inawawia vigumu wao kujiandaa kikamilifu kuelekea mashindano ya Afrika mwezi Desemba na ile ya dunia.

Kocha huyo ameongeza kuwa wachezaji wake wanaendelea kujifua na wana morali ya kupambana katika mashindano hayo hivyo anawaomba wadau mbalimbali kuwasaidia ili waendelee kujiandaa kikamilifu na kuiletea medali Tanzania.