Jumamosi , 11th Jun , 2016

Chama cha Mpira wa Kikapu nchini TBF kimesema kitashirikiana na mchezaji Hasheem Thabiti katika kuendeleza mchezo huo hapa nchini.

Kamishna wa ufundi wa mashindano wa TBF Manase Zabron amesema, upo umuhimu wa vijana ambao wameendelea katika suala la michezo huo kuweza kuwekeza katika miundombinu ya kimichezo.

Zabron amesema, kunahaja ya Hasheem kujenga kuweza kujenga kituo cha kukuza michezo kama wanavyofanya wachezaji wengine katika kuleta maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini.