
Hayo yameelezwa leo na Rais wa TFF Wallace Karia ambapo amesema kuwa mkutano huo utakuwa na Agenda kuu nne ikiwemo Programu ya FIFA.
Mkutano huo utashirikisha nchi 19 na Mwenyekiti wa Mkutano huo atakuwa Rais wa FIFA Gianni Infantino. Wajumbe wa mkutano wanatarajiwa kuwa viongozi wa mashirikisho ya soka kutoka nchi 19 zitakazohudhuria.
Nje na Programu ya FIFA kwa wanachama wake, suala la uwepo wa mashindano ya wanawake, vijana na vilabu, Jinsi ya kuboresha utaratibu wa Uhamisho na Kalenda ya FIFA ni moja ya vipaumbele vitakavyojadiliwa kwenye mkutano huo.