Jumatano , 22nd Apr , 2015

Chama cha mpira wa mikono nchini TAHA kinatarajia kuendesha mafunzo kwa walimu wa shule zote za msingi na Sekondari nchini zinazocheza mchezo huo, taasisi za ulinzi na usalama na waandishi wa habari Julai 7 mpaka 17 Kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza na East Africa Radio, katibu mkuu wa TAHA, Nicholaus Mihayo amesema kozi hiyo inalenga kuwajengea ufahamu na sheria ya jinsi ya kuwafundisha na kucheza na kuandika habari kwa upande wa waandishi wa habari.

Mihayo amesema, mafunzo hayo yatasaidia kukuza mchezo huo lakini pia yataibua vipaji vipya katika ngazi za chini hadi kufikia hatua ya kucheza michuano ya kimataifa.