
luis Suarez akishangilia moja ya magoli aliyoyafunga akiwa Barcelona
Suarez ni moja ya washambuliaji bora duniani, kwa miaka 10 hii ameonesha makali yake akiwa na vilabu vya Ajax ya Uholanzi, Liverpool na Barcelona.
Akiwa na Barcelona, alidumu kwa miaka sita na kufanikiwa kutwaa kombe la Laliga mara 4, kombe la Mfalme mara 4, kombe la Hispania mara 2, kombe la Mabingwa Ulaya mara 1 na kombe la FIFA la dunia kwa ngazi ya vilabu mara 1
UBORA WA SUAREZ UPO WAPI ?
Suarez ni moja ya wachezaji wanaoweza kutengeneza nafasi za kufunga kwa wenzake, na pia ana uwezo wa kufunga yeye mwenyewe, kwa mashuti mazito.
Anafunga magoli kwa aina zote zinazohitajika kwenye soka, ni mzuri kwa kwa kutumia kichwa na pia mzuri kwa matumizi ya miguu yote miwili katika kufunga , jambo lililompa uwezo wa kuifungia Barcelona magoli 198 katika michezo 283.
CHANGAMOTO ZAKE
Matatizo ya Suarez ni ukorofi kwa wachezaji wenzake ikiwemo matukio ya kuwang'ata kama Othman Bakkal, Branislav Ivanovic ,Georgio Chiellin pia ana tuhuma za ubaguzi wa rangi kwa wachezaji weusi hasa kisa chake dhidi ya mchezaji wa zamani wa Manchester Utd Patrice Evra .