Akijibu swali bungeni leo hii naibu waziri wa wizara hiyo Juma Nkamia amesema kutokana na mchango wa shirikisho hilo katika kuendeleza soka la Tanzania wizara yake imekuwa ikilifuatilia suala hilo na kuwa kutokana na kuwa uchunguzi utakapomalizika serikali itatoa tamko rasmi .
Hata hivyo Nkamia amewaasa wale wanaojihusisha na vitendo vya utoaji na upokeaji rushwa katika michezo na kuwa zipo tuhuma ambazo zimekuwepo katika michezo hasa katika mpira wa miguu na kutaka wale wanaojihusisha kuacha mara moja.
Wakati huo huo serikali imesema ina mpango wa kuisaidia timu ya wanamichezo walemavu kutokana na kukumbwa na changamoto ya ukosefu wa fedha mbali na kuwa na wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa wizara ya michezo na utamaduni Juma Nkamia ambapo amesema serikali imeandaa mpango maalumu wa kuwasaidia wana michezo wenye ulemavu ikiwemo kusaidia upatikanaji wa makocha kuwashirikisha katika program za maendeleo ya michezo kujiendeleza katika kushiriki katika mashindano katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Nkamia amesema kuwa kutoka na ufinyu wa bajeti ya wanamichezo serikali inaweka jitihada za kuwasaidia katika kuwasafirisha