Alhamisi , 20th Jun , 2024

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepanda katika viwango vipya vya vifa vilivyotolewa leo Juni 20, 2024 kutoka nafasi ya 119 ya awali mpaka nafasi ya 114

Tanzania imepata alama 1174 tofauti na mwezi uliopita ambapo ilipata alama 1159 ongezeko la alama 15.

Kwa upande wa Burundi imesalia nafasi ya 140 sawa na mwezi uliopita ikiwa na alama 1091.

Nigeria imeporomoka nafasi nane kutoka nafasi ya 30 hadi 38 katika viwango vya FIFA.

Kwa upande wa Afrika,Morocco inaendelea kushikilia usukani nafasi lakini ya kumi na mbili Dunia huku nafasi ya pili ikikamata na Senegal.