Kikosi cha Stars kilimaliza mazoezi yake hapo jana yakiwa ni kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Nigeria Septemba 5 jijini Dar es Salaam kuwania kucheza Afcon.
Kikosi cha Stars kinatarajiwa kuondoka leo jioni nchini Uturuki ambapo kitawasili usiku wa kuamkia hapo kesho ambapo kitaendelea na kambi kwa kufanya mazoezi mepesi siku ya jumatano pamoja wa wachezaji wa kimataifa Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa katika uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya Nigeria.
