
Katika taarifa yake, kocha wa Stars Mart Nooij amesema amekuwa akiwafundisha wachezaji wake kucheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, jambo ambalo wachezaji wameonyesha kufuata vizuri maelekezo yake na kusema wanamuelewa vizuri.
Nooij amesema timu inakwenda kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo, na wanaafahamu wanaenda kucheza ugenini, amewaelekeza vijana wanaocheza nafasi ya ushambuliaji kutumia vizuri nafasi watakazozipata katika mchezo huo.
Nooij amesema katika mpira hakuna kinachoshindikana, kambi ya wiki moja Addis Ababa imewasaidia wachezaji kukaa pamoja na kushika maelekezo yake vizuri, hivyo anaamini timu yake itafanya vizuri katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON.
Nooij amesema, Katika kikosi cha wachezaji wa 22 waliopo kambini jijini Addis Ababa hakuna mchezaji majeruhi, wachezaji wote wako vizuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Mafarao.