Jumanne , 17th Dec , 2019

Wachezaji 8 walioshiriki michuano ya Sprite Bball Kings 2019, ni miongoni mwa wachezaji 15 wa kikosi cha JKT kinacho shiriki kufuzu michuano ya Klabu Bingwa ya Kikapu Afrika iliyo chini ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu duniani FIBA.

MVP Baraka Sadick

Wachezaji hao ni MVP wa Sprite Bball Kings 2019, Baraka Sadick, Mussa Chacha na Cornelius Peter wote wa Mchenga Bball Stars), Stephano Mshana na Denis Chibula wa Tamaduni, Jackson Brown wa Flying Dribllers, Anglebert wa Temeke Heroes na Jonas Mushi wa St. Joseph.

Ufunguzi wa michuano hiyo unafanyika leo nchini Rwanda katika uwanja mpya na wa kisasa kabisa Afrika 'Kigali Arena', ambapo wenyeji Patriots watacheza na JKT mnamo saa 2 usiku.

Timu zinazoshiriki katika zone ya Afrika mashariki ni Patriots(Rwanda), GNBC(Madagascar), Unza Pacers(Zambia) na JKT (Tanzainia) kutoka kundi A, Wakati kundi B lina timu za KPA(Kenya), Ferroviario de maputo(Msumbuji), Cobra(Sudan ya Kusini) na City Oilers(Uganda). 

Timu mbili tu ndizo zitatoka katika makundi hayo zitakazoungana na timu sita ambazo zimevuka katika zone nyingine ambazo kuna timu zimepita kutokana na viwango vya FIBA.

Haya ni makundi ya mashindano hayo.