Jumamosi , 23rd Jul , 2022

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Somalia kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za mataifa barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani CHAN.

Abdul Sopu katika akipongezwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars baada ya kufunga goli

Bao pekee la mchezo huu la Tanzania limefungwa na mshambuliaji Abdul Sopu kwa kichwaa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kibwana Shomari kutoka upande wa kalia wa Taifa Stars kunako dakika ya 46. Kwa ushindi huu Tanzania inahitaji ushindi wa aina yoyote ilikufuzu hatua inayofuata au sare kwenye mchezo wa mkondo wa pili utakaochezwa Julai 30, 2020 uwanja wa Benjamini Mkapa.

Somalia ndio walikuwa wenyeji wa mchezo huu ingawa umechezwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam waliomba wautumie uwanja huu kama uwanja wa nyumbani kutokana na changamoto za usalama nchini Somalia.