Jumatatu , 3rd Oct , 2016

Nyota wa zamani wa Liverpool na West Ham Rigobert Song amekimbizwa hospitalini akiwa katika hali mahututi baada ya kuugua kiharusi.

Song

Song, mwenye umri wa miaka 40, ambaye ni mjomba wa aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, West Ham na Charlton Athletic Alex Song, alichezea timu ya taifa ya Cameroon mechi 137.

Taarifa zinasema alikuwa nyumbani kwake Odza, Yaounde alipopatwa na kiharusi na akakimbizwa hospitalini siku ya Jumapili.

Song, kwa sasa, ndiye kocha mkuu wa timu ya taifa ya Chad, kazi aliyokabidhiwa mwishoni mwa mwaka jana.