Solskjaer aelezea sababu za kumtoa CR7

Jumatano , 15th Sep , 2021

Kocha mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskjer, ameeleza sababu zilizopelekea kufanya mabadiliko ya kuwatoa Cristiano Ronaldo pamoja na Bruno Fernandes katika mchezo uliomalizika kwa kufungwa 2-1 dhidi ya Young Boys kwenye usiku jana wa ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer (mwenye koti jeusi) akiwa na Cristiano Ronaldo baada ya kumtoa na kumuingiza Jesse Lingaard.

Mabadiliko hayo yalifanyika baada ya beki wa kulia wa United, Aaron Wan-Bissaka kupewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Christopher Martins, iliyopelekea mkufunzi huyo kubadilisha mpango pamoja na aina ya uchezaji wa timu yake. 

Solskjear ametabanaisha kuwa alilazimika kufanya hivyo kwakuwa walihitaji kujilinda dhidi ya mashambulizi ya timu pinzani ambapo Ronaldo na Fernandes hakuwa wazuri kwenye nyakati ambazo timu ilipokuwa ikishambuliwa.

Kocha huyo alienda mbali zaidi kwakusema pia alihitaji kuwapumzisha Wareno hao ambao walicheza dakika zote za mchezo wa wikiendi dhidi ya Newcastle pamoja na zile 70 dhidi ya wababe wa Uswizi mjini Bern.