Ijumaa , 21st Mei , 2021

Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni 'Beach Soccer' imeondoka leo kuelekea nchini Senegal kwenye michuano ya 'BSAFCON2021' inayotarajiwa kuanza tarehe 23/5/2021 hadi 29/5/2021

Msafara wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni ukielekea Senegal

Akizungumza kwa kujiamini kocha msaidizi wa timu hiyo Deo Lucas amesema ''tumekianda vyema kikosi chetu na tumepata bahati kundi letu litakuwa na timu mbili tu badala ya tatu, Congo wamejitoa hivyo basi tumebakiwa na Uganda na wenyeji Senegal.''

Aliongezea, ''ratiba ipo ipande wetu, kwa kuwa kabla ya kucheza sisi na majirani wetu Uganda, tutakuwa tumewaona Uganda wanavyocheza na Senegal, kiufundi kwetu sisi itatunufaisha pale tutakapokutana na timu hizi zote mbili.''

Msafara huo wa watu 17 wakiwemo wachezaji 14 makocha 2 kiongozi 1 umeondoka mapema leo Ijumaa wakiwa na ari kubwa ya kufanya vizuri kwa kile kilichoelezwa maadalizi mazuri ya kutosha ikiwemo kambi ya muda mrefu.

Timu hiyo iliyopo chini ya kocha Boniface Pawasa ambaye ni mchezaji nyota wa zamani wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) miongoni mwa wachezaji waliosafiri ni nyota wa zamani wa vilabu vya ligi kuu nchini Tanzania kama Said Morad (Azam) Yahaya Tumbo (Azam), Ismail Gambo (KMC ) Kashiru Salum (Majimaji), Rolland Msonjo ( Mbeya City)