Jannik Sinner Mchezaji namba moja kwa ubora Dunia kwenye mchezo wa tenisi upande wa wanaume.
Sinner ametinga hatua hiyo baada ya kumfunga Daniil Medvedev kwenye mchezo wa robo fainali kwa seti 3-1 yani 6-2, 1-6, 6-1 na 6-4. Katika hatua ya nusu fainali Jannik Sinner ataminyana dhidi ya Jack Draper.
Wakati mpinzani wake Jack Draper amefuzu hatua ya nusu fainali kufuatia ushindi wa seti tatu mfululizo wa 6-3, 7-5, na 6-2 dhidi ya Alex de Minaur. Mchezo wa nusu fainali baina ya Jack Draper dhidi ya Jannik Sinner itafanyika kesho Ijumaa.