Jumanne , 24th Jan , 2017

Golikipa wa Chelsea Thibaut Courtois amesema anafuraha sana kuwepo ndani ya klabu ya Chelsea, na hana mpango wa kuiacha klabu hiyo, ili akacheze ligi ya China.

Courtois

 

Mlinda mlango huyo wa Ubelgiji yupo kwenye kiwango cha hali ya juu kwenye msimu huu, na hakuruhusu bao kwenye michezo 13, akiwa langoni.

Courtois aliyesajiliwa na Chelsea akitokea klabu ya Genk anayocheza Mtanzania Mbwana Samatta mwaka  2011, amesema wakati mwingine huwa anapata wakati mgumu langoni, lakini kwa sasa ameimarika sana.