Ijumaa , 4th Sep , 2015

Simba SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na KVZ usiku wa jana Uwanja wa Amaan Zanzibar katika mchezo wa kirafiki ambapo Simba inajiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu ya Soka Tanzania bara inayoanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu.

Kocha Muingereza, Dylan Kerr hakumtumia kabisa mshambuliaji mpya, Msenegali Pape Abdoulaye N’daw na kwa mara ya kwanza alimuanzisha Joseph Kimwaga aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Azam FC.

Mshambuliaji Mganda Hamisi Kiiza aliisumbua ngome ya KVZ, lakini akashindwa kufunga bao, huku kipa Vincent Angban akiokoa michomo kadhaa ya hatari.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban/Dennis Richard, Emery Nimubona/Hassan Kessy, Hussein Rashid, Said Issa, Samih Nuhu, Justuce Majabvi, Issa Ngoa, Peter Mwalianzi/Danny Lyanga, Joseph Kimwaga/Mwinyi Kazimoto na Hamisi Kiiza/Awadh Juma.

KVZ; Ayoub Bakari, Emil Wiliam, Juma Abdallah/Abdillahi Seif, Iddi Mgeni, Makame Ali, Suleiman Abdulsalam, Masoud Abdallah, Isihaka, Salum Akida, Nasir Bakari na Abbas Abdallah.