
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Klabu ya Yanga Hajji Manara amesema wameomba waandaaji kuangalia ratiba yao kwani Januari Mosi wana mechi dhidi ya Ndanda Fc Mjini Mtwara huku wakiwa wamepangiwa kuanza Michuano ya Kombe la Mapinduzi Januari mbili mwaka huu.
Manara amesema, kama mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Kikosi kimejipanga kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo kwa kuweza kutetea kombe hilo.