Alhamisi , 9th Mar , 2023

Klabu ya Vipers ya Uganda imetangaza kuvunja mkataba na kocha wao mkuu Beto Bianchi hii leo. Taarifa ya klabu hiyo imeeleza.

“Klabu inapenda kumshukuru Bianchi kwa juhudi zake za kutochoka wakati akiwa klabuni hapo na kumtakia mafanikio katika juhudi zake” imeeleza taarifa hiyo.

Vipers wametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram. Kocha huyo amefukuzwa ikiwa imepita miezi miwili tangu kuanza kuiona timu hiyo, baada ya kuchukuwa nafasi ya Roberto Oliveira ambaye kwa sasa anaifundisha Simba.