Simba waomba kuandamana Jumanne

Friday , 21st Apr , 2017

Klabu ya Simba leo imeandika barua kwenda kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuomba kufanya maandamano ya amani siku ya Jumanne ya tarehe 25 mwezi huu

Rais wa Simba, Evans Aveva

Imesema lengo ya maandamano hayo ni ili kupeleka ujumbe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakidai kuwa klabu hiyo imekuwa ikionewa na kutotendewa haki na shirikisho hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Rais wa Simba Evans Aveva ambayo imekwenda kwa jeshi la polisi wameomba kufanya maandamano hayo ya amani ambayo yatakwenda mpaka kwa Waziri na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Katika taarifa hiyo, Simba inaendelea kusisitiza kuwa klabu hiyo imeendelea kuonewa huku malalamiko yake mengi yamekuwa hayafanyiwi kazi kwa haraka.

Hii ndiyo barua yao.......