Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Simba wanacheza mchezo wa 3 leo, ndani ya siku 10

Jumatano , 26th Jan , 2022

Mabingwa wa Tanzania bara Simba SC wanashuka dimba leo jioni kucheza mchezo wa 3 mfululizo ugenini dhidi ya Kagera Suga katika dimba la Kaitaba huko Bukoba mkoani Kagera. Mchezo huu ni wa kiporo na unachezwa Saa 10 jioni.

(Kiungo wa Simba SC, Clatous Chama akicheza dhidi ya Mtibwa Sukari)

Mchezo wa Jioni ya Leo ni wa 3 mfululizo kwa Simba SC wanacheza ugenini ndani ya siku 10. Katika mfululizo wa michezo hii Simba walicheza jijini Mbeya dhidi ya Mbeya City Januari 17, 2022 mchezo wa walifungwa bao 1-0. Januari 22 walicheza na Mtibwa Sugar mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu 0-0.

Kwa upande wa Kagera Sugar nao wanarejea kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Kaitaba baada ya kucheza michezo miwili ugenini mfululizo ambao walitoka sare ya mabao 3-3 na Biashara United Januari 15 na Januari 21 walicheza na Dodoma Jiji na walishinda kwa mabao 2-1.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana kwenye uwanja wa Kaitaba Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 mchezo ambao ulichezwa Aprili 21, 2021 na mabao ya wekeundu wa msimbazi kwenye mchezo huo yalifungwa na Chris Mugalu na Luiz Miquissone.

Kagera Sugar wapo nafasi ya 11 wakiwa na alama 13 kwenye michezo 12 na mchezo wa jioni ya leo ni wa kipora mchezo wa raundi ya 9 ambao haukuchezwa hapo awali baada ya wachezaji wa Simba kuumwa mafua. Simba SC wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 25 utofauti ya alama 10 dhidi ya Yanga wenye alama 35. 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya