Ijumaa , 13th Mei , 2022

Klabu ya Simba imetangaza kumpa mapumziko ya hadi mwisho wa msimu nyota wake Bernard Morrison huku ikimshukuru na kumtakia mafanikio mema katika safari yake ya soka hapo baadae

Taarifa ya Klabu hiyo imeeleza kuwa mapumziko hayo ni kwa ajili ya kumpa nafasi mchezaji huyo kushughulikia mambo yake binafsi

Simba imemshukuru nyota huyo kwa mchango wake katika Klabu hiyo na mafanikio aliyoyaleta ikiwemo kushiriki robo fainali ya michuano ya Shirikisho barani Afrika