Simba SC yashinda kwa shida dhidi ya Mwadui

Jumapili , 18th Apr , 2021

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania klabu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mwadui FC, kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga jioni ya leo Aprili 18, 2021.

Goli la John Bocco dhidi ya Mwadui FC

Simba ililazimisha kusubiri mpaka kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwana kumalizika kwa timu kutoshana nguvu kabla ya nahodha John Bocco kuingia na kuifungia Simba SC goli pekee la ushindi dakika ya 66.

Goli la John Bocco  limeiwezesha Simba SC kufikisha pointi 52 katika nafasi ya 2 nyuma ya Yanga SC yenye pointi 54 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Bocco pia ameendeleea kujiweka vizuri kwenye mbio za ufungaji bora baada ya kufikisha magoli 10 akiwa sawa na mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube wote wakiwa nyuma ya Meddie Kagere mwenye magoli 11.