Kauli hiyo imethibitishwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmedy Ally kuwa kukosekana kwa wachezaji kama hao ni pengo kubwa lakini Simba ni timu kubwa na pia inawachezaji wengi.
Mchezo huo utakaosimamiwa na Mwamuzi Hery Sasii utachezwa majira ya saa 2:30 usiku utakuwa wa tano kwa Azam Fc wenye pointi 8 baada ya mechi nne huku ukiwa mchezo wa tatu kwa Simba Sc wenye alama 6.
Azam Fc imepoteza mara mbili mfululizo kwenye mechi zilizopita dhidi ya Mnyama wakipoteza 3-0 kwenye Ligi mnamo Mei 9, 2024 kwa magoli ya Sadio Kanoute, Fabrice Ngoma na David Kameta ‘Duchu’ baada ya kupoteza 1-0 kwenye fainali ya kombe la Muungano 2024 kwa bao pekee la Babacar Sarr.