
Chama akipokea tuzo kutoka kwa mgeni rasmi Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ni Clatous Chama wa Simba SC.#TuzoVPL @VodacomTanzania pic.twitter.com/dc9LUiwqox
— EastAfricaTV (@eastafricatv) August 7, 2020
Tuzo ya Heshima imeenda kwa nguli wa soka wa zamani ambaye pia ni baba mzazi wa msemaji wa Simba SC Haji Manara, Mzee Sunday Manara.
Kiungo Bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ni Clatous Chama wa Simba SC.
Beki Bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ni Nicolaus Wadada wa Azam FC.
Mwamuzi Bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ni Ramadhan Kayoko.
Mwamuzi Bora msaidizi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ni Frank Komba.
Tuzo ya Golikipa Bora wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 imeenda kwa kipa wa mabingwa Aishi Manula.
Tuzo ya Golikipa Bora wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 imeenda kwa kipa wa mabingwa Aishi Manula.#TuzoVPL @vodacomtanzania pic.twitter.com/XngDXGe1LB
— EastAfricaTV (@eastafricatv) August 7, 2020
Tuzo ya Kocha Bora wa mwaka wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20, imeenda kwa kocha wa mabingwa Simba SC Sven Vandenbroeck.
Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 imeenda kwa Novatus Dismas wa Biashara United.
Tuzo ya Mfungaji bora wa Ligi Kuu imeenda kwa Meddie Kagera
Kikosi Bora cha msimu VPL 2019/20.
1. Aishi Manula
2. Nicolas Wadada
3. David Luhende
4. Bakari Mwamnyeto
5. Pascal Wawa
6. Zawadi Mauya
7. Chama
8. Luis Miquissone
9. Lucas Kikoti
10. Maddie Kagere
11. John Bocco