
Wakizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwa upande wa jiji la Dar es salaam, mmoja wa watoto Lucia Gasper amesema, michezo inaelimisha na pia kumchangamsha mtoto hivyo wazazi wananatakiwa kuwapa watoto uhuru lakini usipitilize hususani watoto wa kike ambao baadhi ya maeneo hapa nchini wananyimwa haki ya kupata elimu.
Kwa upande wake mtoto Festo Frank amesema, wamefurahi kujumuika kwa pamoja kwa ajili ya michezo hivyo wazazi wanatakiwa kuwaruhusu watoto kucheza kwa sababu nihaki yao.
Frank amesema, watoto pia wanapopata haki ya kuweza kushiriki michezo wanatakiwa kuangalia pia na makundi aliyonayo yasiwe ya kupotosha.
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani.
Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika ambapo elimu kwa watoto ndio imekuwa mada kuu kwa nchi nyingi katika kumuinua mtoto wa Africa.