Ijumaa , 2nd Feb , 2024

Meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa Mlinde Mahona amesema kuwa matengenezo katika maeneo mbalimbali ndani ya uwanja yanaendelea vyema na anaridhishwa na kasi ambayo inaendelea kwa mkandarasi .

Mahona amesema kuwa mafundi wanaendelea na kazi ya kutoa uchafu wote kwenye kuta za uwanja huo huku hatua inayofata ni uwekaji wa viti vipya ndani ya uwanja wa Mkapa.

’Tumeshaoneshwa mfano wa viti ambavyo vitawekwa na vipo kiwanda vinamaliziwa na hivi karibuni vitakuja Tanzania ‘’ amesema Mahona

Aidha Meneja Mahona ametoa raia kwa wanamichezo wanatumia uwanja huo  kuwa wastarabu pindi wanapokuja kutazama timu zao.

Ikumbukwe kuwa mwaka jana 2023 Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ilisaini  Mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao utagharamia  zaidi ya Sh. Bilioni 31 na utarajiwa kukamilika Julai 2024.