
Kelvin John katikati akishangilia na wachezaji wenzake wa Serengeti Boys
Mchezo huo utakaoanza majira ya saa 11 jioni unazikutanisha Serengeti Boys ambayo ilianza safari yake kwa ushindi dhidi ya Burundi wa mabao 2-1, baadaye ushindi wa 5-0 shidi ya Sudan na 4-0 dhidi ya Rwanda huku Uganda ikishinda 1-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ethiopia, 3-1 dhidi ya Kenya na 6-1 dhidi ya Sudan Kusini.
Gunzo kubwa katika michuano hiyo ni mshambuliaji wa Serengeti Boys, Kelvin John ambaye ameonekana kung’ara katika michezo yote aliyocheza mpaka sasa, akiwa amefunga mabao sita katika michezo mitatu ikiwemo hat-trick katika mchezo dhidi ya Rwanda.
Kiwango cha mchezaji huyo kimewavutia wengi miongoni mwa wadau wa soka wakimtabiria kufanya vizuri zaidi endapo ataendeleza kiwango hicho mbeleni na kuwa tegemeo kwa timu ya taifa, Taifa Stars.
Mchezo mwingine wa nusu fainali ambao utachezwa mapema saa nane mchana ni kati ya Ethiopia na Rwanda ambapo mechi zote zikichezwa katika uwanja wa taifa.