Jumanne , 3rd Jan , 2017

Serena Williams ameshinda mechi yake ya kwanza tangu atoke kwenye Mashindano ya US Open baada ya leo kumshinda Pauline Parmentier katika michuano ya ASB Classic jijini Auckland, nchini New Zealand.

Serena Williams

 

Serena, ambaye amechumbiwa hivi karibuni, alikuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili ya mwisho ya msimu wa 2016 kutokana na jeraha la bega na hajacheza mechi yoyote tangu Mashindano ya US Open katika mwezi wa Septemba mwaka jana lakini ameshinda mechi yake ya kwanza ya mwaka 2017 kwa seti za 6-3, 6-4.

Akiongea baada ya mechi hiyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 35, amemsifu  mpinzani wake kwa kuonesha ushindani na mchezo mzuri