
(Kocha wa Yanga, Mohammed Nasreddine Nabi)
“Yanga wana ukame wa kutwaa taji ndani ya misimu mine, nimefuatilia na nimebaini mapungufu ndani ya misimu hiyo ni ufinyu wa kikosi na kukosa mastaa wenye mwendelezo wa ubora kitu ambacho msimu huu anacho,” alisema Nabi
“Nafurahi msimu huu nimeikuta timu nzuri na ina kikosi kipana ambacho akikosekana mmoja mwingine anachukua nafasi na anafanya kile kinachotakiwa kufanywa,” aliongeza Kocha huyo.
Nabi alisema Yanga ya msimu huu imekuwa na mfululizo wa majeruhi lakini hakuna pengo linaloonekana tofauti na misimu iliyopita na aliongeza kuwa mastaa wake wana ari ya ushindani.
Yanga ndio vinara wa ligi hiyo baada ya kucheza michezo 14 ya mzunguko wa kwanza na kukusanya pointi 36 wakiwa mbele pointi tano na watani zao Simba walio nafasi ya pili na pointi 35.