
Ronaldo de Lima.
Real Madrid na Barcelona wanapewa nafasi ya kushinda ubingwa wa klabu bingwa ulaya lakini wanahitaji kupambana na kuwa bora zaidi mbele ya timu hizo, kulingana na gwiji huyo wa soka.
Timu hizo za Laliga zimetawala klabu bingwa ulaya kwa miaka ya karibuni, ambapo Real Madid wameshinda mara nne huku Barcelona wakishinda moja katika miaka mitano. Liverpool ilikaribia kuvunja umwamba wao msimu uliopita lakini iliishia kuchapwa 3-1 dhidi ya Real Madrid katika fainali mjini Kiev.
Ronaldo ambaye aliichezea Barcelona msimu wa 1996-97 na Real Madrid kati ya mwaka 2002 na 2007 anaamini klabu moja wapo inaweza kushinda kombe hilo lakini akizipa nafasi kubwa timu za Uingereza kushinda ubingwa wao wa kwanza tangu Chelsea ilipofanya hivyo mwaka 2012.
“ Timu nyingi zimejiimarisha sana, mashindano haya ni magumu, unatakiwa ufahamu namna ya kucheza “. Amesema Ronaldo de Lima.
“ Timu za Hispania zinafahamu vizuri namna ya kucheza katika michuano hii, lakini ninaamini msimu huu zitapata changamoto kutoka kwa timu za Uingereza kwasababu wako vizuri na wana nguvu kubwa ya fedha za kununua na kuuza wachezaji, ninaamini watafanya hivyo “. Ameongeza.